Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 30Article 554404

Habari Kuu of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Sio kila kitu lazima tuwalipishe wananchi"- Waziri Ummy

Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, amewataka Wakuu wa Mikoa wote pamoja Wakurugenzi wa Halmashauri nchini, kujitahidi kuendesha na kujenga miradi ya maendeleo na uchumi pasipokuwa kuwalipisha fedha wananchi kila mara.

Ametoa kauli hiyo akiwa katika ziara yake wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, alipotembea miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na mabanda ya wafanya biashara wadogo wadogo wilayani humo.

"Si kila tukitaka ardhi lazima tuuwalipishe wananchi, tuwabanae Wakurugenzi wetu, sio kila kitu lazima wanachi wetu walipie ili kujenga miundo mbinu, nisistize tu Rais hajapiga marufuku kupanga miji, ila alichosema ni kuwa tunapowatoa watu kwenye makazi yao tujue wanapelekwa wapi" Waziri Ummy

Alifafanua Mkakati huo wa kuboresha miradi ya maendeleo kufuatia agizo la Rais Samia, linalowata Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha wanapanga miji katika taratibu zilizowekwa kiufanisi, na sio kuwaamisha wananchi kisha kuwatelekeza pasipo makazi.