Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573745

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sirro: Pikipiki Kwenye Vituo vya Polisi Tutazipiga Mnada

IGP Sirro IGP Sirro

MKUU wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema Jeshi la polisi limepokea agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuondoa pikipiki katika vituo vya polisi na kwamba Jeshi litaandaa mkakati ikiwa ni pamoja na kuzipiga mnada pikipiki zote kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

IGP Sirro amesema hayo leo Jumanne, Novemba 23, 2021 wakati akizungumza kwenye hafla ya Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo Rais Samia alikuwa mgeni rasmi.

Afande Sirro amesema idadi kubwa ya pikipiki katika vituo hivyo zimetelekezwa na wamiliki baada ya kukamatwa wakati wa oparesheni za kawaida za jeshi hilo.