Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 19Article 572794

Habari Kuu of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sirro awashukia wanaokata viungo vya binadamu

Sirro awashukia wanaokata viungo vya binadamu Sirro awashukia wanaokata viungo vya binadamu

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema yoyote atakayekutwa amekata kiungo cha binadamu mwenzake kwa lengo la kujipatia utajiri atamshughulikia kwa mujibu wa sheria akisema kufanya hivyo ni unyama na ushamba.

Ametoa onyo hilo leo Ijumaa Novemba 19, 2021 wakati wa ziara yake ya kukagua jengo la ofisi za Jeshi la Polisi zinazojengwa wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Kauli ya IGP Sirro imekuja siku chache baada ya tukio la kufukuliwa kwa maiti ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) na kukatwa mguu na watu waliokamatwa na kukiri kufanya hivyo katika Halmashauri ya Bumbuli.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi halina muhali na muhalifu wanaofanya matukio hayo kwani huo ni ushamba wakudanganywa na waganga wa kienyeji kuwa kupata utarijiri lazima ukate kiungo cha binadamu.

"Acheni kudanganywa na waganga wa kienyeji sababu mganga atakupaje utajiri wakati yeye mwenyewe ni masikini? nyumba anayokaa haieleweki na wala hajasomesha watoto wake " Amesema Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi huku akisisitiza Jeshi hilo lina timu ya kupambana na mauaji ya aina zote .

Amesema mtu akipelekwa mahakamani kwa kosa hilo la kukata kiungo cha binadamu atanyongwa kwa kuwa mtu huyo ni mnyama hivyo lazima ashughulikiwe.

"Suala la kukata viungo unategemea kuwa tajiri vilishapitwa na wakati halafu ni ushamba, unakata mtu kiungo maana yake anakufa tukikukamata adhabu yake ni kunyongwa" amesema IGP Sirro

Amewaomba viongozi wa dini na wanasiasa kusaidi kutoa elimu kwa jamii ili waache na hizo Imani.