Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 08Article 546133

Habari Kuu of Thursday, 8 July 2021

Chanzo: ippmedia.com

Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa - Samia

Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa - Samia Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa - Samia

Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 8, 2021 Mjini Morogoro wakati akifungua mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT) aliposema wakati mwingine dini na siasa vinaenda sambamba.

Amesema licha ya kuwa unaweza kutumikia dini na kuwa mwanasiasa, lakini vibaya unapotumia siasa kwenye dini.

Amewaomba viongozi wa dini kushirikiana na serikali katika kudumisha amani na usalama wa nchi uliopo.

Amesema ni nafasi ya viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali yakitaifa ikiwemo suala la kuhesabiwa sensa linalotarajia kufanyika mwezi Agosti mwakani.

"Nawasihi viongozi wa dini kuwasihi wananchi kuachana na imani potofu na kushiriki kwenye sensa, suala la sensa lipo hadi kwenye vitabu vya dini na hivyo sio suala geni kwetu," amesema.

Rais Samia pia amewataka viongozi wa dini kote nchini kuhubiri amani, upendo na mshikamano huku wakizidi kuliombea Taifa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Katika risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT), Baba Askofu Dk. Alinikisa Cheyo, ameomba serikali kuondoa kodi ya mapato (Income Tax) kwenye shule na huduma za afya zinazotolewa na taasisi za kidini nchini.

“Tunaiomba Serikali ifikirie kuziondolea Taasisi za kanisa kodi za mapato (income tax) ili taasisi hizo ziweze kujiendesha kwani hazipati faida kubwa na ile faida ndogo inayoipata inatumika kughramia uendeshaji wa huduma hizo,” amesema Askofu Cheyo.