Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 27Article 553993

Siasa of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Slaa aitikia wito kabla ya kukamatwa

Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga

Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa amefika katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa baada ya jana Kamati hiyo kutoa ombi kwa Spika wa Bunge Job, Ndugai kutaka akamatwe.

Kamati hiyo iliomba kukamatwa kwa mbunge huyo na kufikishwa katika kikao cha kamati saa 4.00 asubuhi leo Ijumaa Agosti 27, 2021.

Silaa aliitwa kuhojiwa kwa mara ya kwanza katika kamati hiyo Agosti 24, 2021 akituhumiwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.