Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553408

Siasa of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Slaa awasili kwenye Kamati ya Maadili

Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga

Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa amewasili kuhojiwa na Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku akikataa kusindikizwa na askari polisi kama ilivyokuwa kwa mwenzake, Askofu Josephat Gwajima aliyehojiwa jana.

Baada ya mabishano yaliyodumu kwa dakika kadhaa Silaa alikubali kuongozana na askari hao kuelekea ukumbini ambako mahojiano yalitarajiwa kufanyika.

Silaa amewasili bungeni hapo baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuwatumia wito wabunge hao kuhojiwa na kamati hiyo kwa kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge. Ndugai alitoa amri hiyo Jumamosi iliyopita.

Silaa amewasili bungeni saa 6:49 mchana akiwa kwenye gari jeusi sawa na suti aliyoivaa huku mkononi akisukuma sanduku jeusi pia.

Akiwa katika geti kubwa la kuingilia, Silaa alikataa kuongozana na askari wawili kama ilivyo utaratibu akitaka aonyeshwe kanuni inayotaka mbunge kusindikizwa anapoenda kuhojiwa na kamati.

Hawa najua (waandishi wa habari) wapo kwa mujibu wa kanuni, hawa pia (maofisa usalama wanaolinda getini) wapo kwa mujibu wa kanuni, niambie kanuni gani inayonitaka niongozane nao".

Hata hivyo, Ofisa Mwandamizi wa Usalama bungeni, Peter Magati, alimweleza Silaa kuwa Bunge huendeshwa kwa utaratibu, kanuni, sheria na miongozo ambavyo kila anayeingia ndani ya viunga hivyo anapaswa kuvizingatia.

Baada ya maelezo hayo Silaa alikubali kuongozana na askari hao mmoja akiwa amevaa kiraia na mwingine sare za polisi hadi katika viti vilivyokuwa karibu na mashine ya kukagulia watu wanaoingia jengo la utawala la Bunge.

Mgomo kama huo ulifanywa jana na Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima mara tu alipoingia kwenye ukumbi ambako mahojiano yalifanyika.