Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 06Article 555670

Siasa of Monday, 6 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Spika Ndugai ampongeza Waziri Gwajima kwa hili

Spika Ndugai ampongeza Waziri Gwajima kwa hili Spika Ndugai ampongeza Waziri Gwajima kwa hili

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amempongeza Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, kwa hatua alizozichukua dhidi ya mtoto wa miaka 9 mkoani Mwanza aliyekatisha masomo na kuanza kumuuguza Bibi yake anayeugua saratani.

Spika Ndugai ameitoa kauli hiyo leo Septemba 6, 2021, Bungeni Dodoma.

"Nakushukuru sana Mh. Waziri kwa kufika Mwanza kwa yule binti wa miaka 9 na tunashukuru kwa hatua ambazo mmezichukua ni stori inayosikitisha sana," amesema Spika Ndugai.

Hivi karibuni iliripotiwa taarifa ya mtoto wa miaka 9 anayemhudumia Bibi yake ambaye ni mgonjwa hali iliyopelekea kukosa masomo huku wazazi wake nao wakiwa hawajawahi kumtafuta tangu alipoenda Mwanza kumsalimia Bibi yake huyo akitokea Zanzibar, ambapo mara baada ya taarifa hiyo Waziri Gwajima alienda Mwanza na kusaidia mtoto huyo kurudi tena shule.