Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554674

Siasa of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Spika Ndugai aomba radhi Wakristo kwa kauli ya "Mke wa Yesu"

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ameomba radhi waumini dini ya kikristo na Watanzania wote waliokwazika na kauli yake aliyoitoa leo asubuhi akieleza mstari wa Biblia.

Akizungumza bungeni leo Agosti 31, Spika Ndugai amesema ameshatembelea Uyahudi na kwamba anajua maeneo aliyozaliwa Yesu.

“Uyahudi nimekwenda mara nne, nimefika Kapernaumu kule kwenye kijiji cha Yesu, Galilaya yote ile nimetembea naijua, Kana naijua.

“Nimefika Nazareth, najua unaposema Yesu alitembea na mke wake kutoka Nazareth kwenda mpaka Yerusalem kuhesabiwa na wakakosa mahali pa kulala kutoka Yerusalem kwenda mpaka Betlehem alipozaliwa Yesu, distances zote zile nazijua.”

Hata hivyo, katika taarifa iliyotolewa leo Agosti 31, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, ofisi ya Bunge imefafanua kuwa, Spika Ndugai alimaanisha; “Yusufu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda Yerusalem kuhesabiwa na siyo Yesu kama alivyotamka awali.

“Hivyo, kilichotokea ni hali ya kibinaadamu ya ulimikuteleza ambayo huweza kumtokea mtu yeyote yule,” imefafanua taarifa hiyo.