Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552556

Siasa of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Spika Ndugai ataka Wabunge viti maalum kupigiwa kura

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Spika wa Bunge Job Ndugai, ameutaja mfumo wa kuwachagua wabunge wa viti maalum na kundi la wenye ulemavu hauna urafiki kwa wawakilishi na wanaowakilishwa.

Spika Ndugai amesema utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti maalumu unapaswa kubadilishwa hasa kundi la walemavu.

Spika Ndugai amesema utaratibu wa sasa ambapo wenye ulemavu wanapigiwa kura na kundi la wanawake wote si mzuri.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 19,2021 Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la walimu wenye ulemavu ambalo limewakutanisha wawakilishi wa wenye ulemavu nchi nzima.

Spika amesema wakati mjadala wa ubunge wa viti maalumu ukiendelea kuhusu namna ya upatikanaji wa wawakilishi hao ama kufuta nafasi hizo, wenye ulemavu wanapaswa kuvhaguana wenye.

"Tunao wabunge wanaowakilisha kundi la wenye ulemavu lakini kuchaguliwa kwao hakuwahusishi kundi hilo moja kwa moja, Sasa lazima tuangalie hili," amesema Ndugai.

Akizungumza kuhusu kundi la walimu wenye ulemavu, amewataka kujiamini na kufanya kazi kama ilivyo kwa watumishi wengine badala ya kulalamika ambako hakuwezi kuwasaidia kitu.

Hata hivyo Ndugai akisisitiza kwa walimu kufanya shughuli zingine katika kujiongezea kipato ikiwemo kilimo na biashara ndogo ndogo kwakuwa maisha si magumu kwa mwenye kuhangaika.