Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541789

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Spika wa Bunge la Tanzania awaonya wabunge dhidi ya usherati

- Spika wa bunge la Tanzania amewaonya wabunge wa kiume dhidi ya kuwanyemelea wake wa wenyewe

- Ndugai alitoa onyo hii baada ya madai kuibuka kwamba kumekuwa na visa vingi vya wabunge kuwanyemelea wapenzi wa wenyewe

- Haya yanajiri baada ya mbunge mmoja kutoka Arusha kukatiza sherehe ya harusi mbunge mmoja akilalamamikia kuibiwa mume

Spika wa bunge la kitaifa la Tanzania Job Ndugai amewaonya wabunge dhidi ya kuwanyemelea wapenzi wa wenyewe ambao wako tayari kwenye ndoa.

Ndugai aliyasema haya baada ya kuibuka madai kwamba visa vya usherati miongoni mwa wabunge vimekithiri sana.

Kwa mujibu wa taarifa za Daily Nation, Ndugai aliwaonya wabunge dhidi ya kuwanyemelea wapenzi wa wenyewe haswa walioko katika ndoa baada ya mbunge kutoka Arusha kusimamisha harusi.

Mbunge Catherine kutoka eneo la Magige anasemekana kusimamisha harusi ya Kuzula Madoda akidai kwamba alikuwa mpenziwe.

Madoda anasemakana alikuwa ameandaa harusi iyo kisiri.

Join our Newsletter