Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541405

Habari za Biashara of Monday, 7 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Stanbic yaibeba Taswa SC kuIvaa Bunge FC

Stanbic yaibeba Taswa SC kuIvaa Bunge FC Stanbic yaibeba Taswa SC kuIvaa Bunge FC

Taswa SC inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge FC ambapo Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki ya Stanbic Tanzania, Desideria Mwegelo, amesema msaada huo utafanikisha vema ziara hiyo ya jijini Dodoma.

Mwegelo alisema benki yao  inatambua mchango wa Taswa SC katika maendeleo ya michezo nchini pamoja na masuala ya afya.

“Michezo ni moja ya njia ya kujenga afya ya mwili katika jamii. Benki yetu mbali ya kusaidia michezo, pia inasaidia masuala ya afya, tunaamini kwa msaada huu, timu itafanya vizuri katika mchezo huo,” alisema Mwegelo.

Alisema benki yao inajisikia fahari zaidi kushirikiana na Taswa SC kwa kuwa  hufanya hivyo hiyo ikiwa ni mara ya pili.

“Msaada huu pia ni sehemu ya Benki ya Stanbic Tanzania kujishughulisha na shughuli za kijamii. Tunawaomba wachezaji wa Taswa SC watuwakilishe vizuri siku ya mchezo huo,” alisisitiza Mwegelo.

Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary, aliipongeza Benki ya Stanbic Tanzania kwa msaada huo ambao utwafanya kufanya safari yao kwa uhakika zaidi mbali ya kucheza mechi hiyo.

Majuto alisema klabu hiyo ilikuwa njiapanda kusafiri kwenda Dodoma na kwamba  msaada huo umewahamasisha wachezaji kufanya vema.

“Msaada umekuja wakati muafaka ambapo klabu ilikuwa inahitaji kusafiri na kucheza mechi dhidi ya timu ya Wabunge. Naishukuru sana kwani ndoto yetu ya miaka mingi kucheza na Bunge FC jijini Dodoma itatimia,” alisema Majuto.

Michezo

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni