Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 18Article 558190

Habari za Mikoani of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: Channelten

Stendi mpya kujengwa Mkuranga

Waziri wa Tamisemi ,Ummy Mwalimu Waziri wa Tamisemi ,Ummy Mwalimu

Waziri wa nchi ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Ummy Mwalimu amewahakikishia wananchi wa Mkuranga kuwa serikali ipo mbioni kujenga Kituo kikubwa cha mabasi kitakachoitwa MAMA SAMIA SULUHU HASSAN kwaajili ya mabasi yaendayo mikoa ya kusini .

Ummy amesema hayo baada ya ombi lililotolewa na mbunge wa jimbo la mkuranga ambaye pia ni Naibu waziri mifugo na uvuvi Abdalah Ulega , ambaye alimweleza Waziri hiyo kuwa wananchi wamekuwa wakilandalandala kwa kukosa huduma ya kituo cha mabasi , kutokana na ufinyu kituo cha mbagala rangi tatu.

Ummy Mwalimu amesema hayo katika ziara yake inayoendelea mkoani Pwani ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu , madaraja na barabara.