Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552667

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TAMISEMI yakanusha kusitisha "Elimu Bure"

Sera ya Elimu bure Tanzania Sera ya Elimu bure Tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu, Amekanusha madai yanayoendelea kuhusu kufutwa kwa elimu bure kwa ngazi ya shule ya msingi na sekondari kuwa hayana msingi na sio ya kweli kwani serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu .

Amesisitiza kuwa, mpango wa serikali, katika kuboresha na kufanya mapinduzi katika sekta ya elimu ni pamoja na kutoa elimu bure ili kuwapa mwanya watoto wote nchini kupata elimu kwa ajili ya ukombozi wa taifa zima.

"Kumekuwa na maneno yanaendelea kwamba kuna uwezekano wa kufuta elimu ya msingi bila ada, sio kweli,ni uzushi, na serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu ya msingi na sekondari, kwa hiyo sera hii ya elimu msingi bila ada itaendelea kutekelezwa"

Sera ya elimu bure ilianza kufanya kazi katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne iliyokuwa chini ya Mstaafu Jakaya Kikwete ikiwa imejikita zaidi kwenye elimu ya msingi na hapo baadae katika seriklai ya awamu ya tano chini ya Hayati Magufuli, wigo wa elimu bure ulipanuka na kufikia elimu ya sekondari kwa maana ya kidato cha kwanza hadi cha nne.