Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559960

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TAMISEMI yathibitsha kutoa bilioni 298 kwa Halmashauri zote

Ummy Mwalimu, Waziri TAMISEMI Ummy Mwalimu, Waziri TAMISEMI

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, amesema kuwa tangu mwezi June, 2021 Halmashauri zote nchini zimepokea takribani bilioni 298 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

ametoa taarifa hii wakati wa Mkutano Maalum wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania-ALAT, unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, leo tarehe 27 Septemba, 2021.

Waziri huyo pia amezungumzia tabia ya baadhi ya Watendaji wa Halmashauri kutumia vibaya fedha za mapato kinyume cha taratibu za kiutendaji, na kusema kuwa atawabana ipasavyo.

"Kwa sababu Rais ananipima kwenye ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za mapato ya ndani, nimewaambia (Wakurugenzi) nitawabana, sitakubali mimi nitumbuliwe wakati wao wapo na wanachezea fedha za wananchi".Waziri Ummy Mwalimu.