Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 05Article 583381

Habari Kuu of Wednesday, 5 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

TANESCO Yatangaza Bei Mpya za Kuunganisha Umeme

TANESCO Yatangaza Bei Mpya za Kuunganisha Umeme TANESCO Yatangaza Bei Mpya za Kuunganisha Umeme

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limetangaza gharama mpya za kuunganisha umeme, ambapo vijijini ni shilingi 27,000 kwa wateja wa njia moja bila kujali umbali wala idadi ya nguzo na kwa mjini gharama zinaanzia shilingi 272,000 kwa kutegemea umbali toka unapochukulia umeme na idadi ya nguzo.

Taarifa ya Taneso inasema kwa mteja wa mjini kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960 kwa mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618 umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670.

Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014 kwa mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385, umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156.