Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572455

Habari Kuu of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

TANESCO watangaza upungufu wa umeme nchini

TANESCO watangaza upungufu wa umeme TANESCO watangaza upungufu wa umeme

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limetoa taarifa ya upungufu wa maji kwenye mabwawa yanayozalisha umeme nchini. Kwa mujibu wa TANESCO imeeleza kuwa baada ya kutokea hali ya mabadiliko ya hali ya hewa, kiwango cha maji katika mito na mabwawa yetu kimepungua kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na hali hiyo ya upungufu wa maji, uzalishaji wa umeme umeathirika katika vituo vya kuzalisha umeme vinavyotumia maji ambapo athari kubwa zimetokea katika vituo vya Kihansi, Kidatu na Pangani.Jumla ya upungufu wa uzalishaji ni takribani 345MW, ambayo ni asilimia 21 % ya uzalishaji wote.

Shirika linachukua hatua za haraka kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia, kwa kuharakisha matengenezo ya baadhi ya mitambo yake ya Ubungo I (25MW), upanuzi wa Kinyerezi I (185MW) na Ubungo Ill (112MW) pamoja na kuwasha kituo cha Nyakato (36MW). Hii itaongeza jumla ya 358MW.

Kwakuwa kutakuwa na upungufu kwa baadhi ya mikoa taarifa zitatolewa kwa wakati iii wateja wetu waweze kupanga kazi zao.

IMETOLEWA NA TANESCO MAKAO MAKUU