Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540379

xxxxxxxxxxx of Friday, 28 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

TARURA wameagizwa kufuata vipaumbele vya madiwani

Mwalimu amebainisha hayo leo, wakati akikagua ujenzi wa miundombinu ya barabara Manispaa ya Shinyanga.

Amesema katika Bajeti ya mwaka wa fedha (2021-2022) unaoanza Julai, wakala hao ni marufuku kutekeleza miradi ya miundombinu ya barabara bila ya kupitishwa na madiwani.

"Wizara tumeshatoa muongozo, kuwa kwenye Bajeti ya Julai TARURA mtajenga miundombinu ya barabara kwa kufuata vipaumbele vya madiwani,"amesema Mwalimu.

Aidha amesema  katika fedha ambazo zimetolewa kwa ajili ya matengenezo ya barabara Manispaa ya Shinyanga Sh. bilioni 1.4 Rais Samia ameongeza Sh. milioni 500, na hivyo kufanya jumla kuwa Sh. bilioni 1.9.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, alimuahidi Waziri huyo kuwa maagizo yote ambayo yametolewa atayafanyia kazi.

Aidha Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, amesema Jambo hilo ni jema, ambalo litasaidia kumaliza changamoto za ubovu wa barabara hasa kwenye maeneo korofi, kutokana na madiwani ndiyo wanafahamu barabara zenye matatizo makubwa.

Join our Newsletter