Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 19Article 547549

Diasporian News of Monday, 19 July 2021

Chanzo: ippmedia.com

TASAF yamkosha Waziri wa Zanzibar

TASAF yamkosha Waziri wa Zanzibar TASAF yamkosha Waziri wa Zanzibar

Kutokana na hali hiyo, ameahidi kuchukua ujuzi huo ili kusaidia utekelezaji wa miradi visiwani humo.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipoongoza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea miradi inayotekelezwa na TASAF kwa walengwa wilayani Chamwino.

Alisema ujumbe wake umeenda kujifunza ili kutekeleza mpango huo kwa ufanisi kama ilivyo Tanzania Bara.

“Tumejifunza vitu vingi kwa wenzetu katika utekelezaji wa miradi ya TASAF… wanastahili pongezi kwa sababu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, na sisi kwa vile ni awamu ya kwanza tumepata ujuzi wa kwenda kuboresha mpango wa utekelezaji,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamaja, alisema katika awamu ya sasa wamejipanga kujikita zaidi katika utoaji ajira za muda kwa sababu zina manufaa makubwa.

Alisema utekelezaji wa awamu ya tatu ya mpango wamejipanga kutoa ajira za muda katika mashamba ya zabibu ambayo ni mashamba darasa.

“Hizi ajira za muda mfupi zimeleta manufaa katika awamu iliyopita kutokana na wengi wa vijana walikwenda kuanzisha mashamba yao,” alisema.

Alisisitiza: “Tunafikiria katika awamu hii tujikite zaidi kufanya hivyo kwa sababu tumeona ajira za muda zinaleta matokeo chanya, walengwa wanajikwamua na kuanzisha mashamba yao binafsi.”

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Chamwino, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino, Athuman Masasi, alisema miradi 502 imetekelezwa katika vipindi vya miaka minne kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2018/19.

Alisema aina ya miradi iliyotekelezwa ni upanuzi, ukarabati na ujenzi wa malambo 305, vitalu vya miche ya miti ya zabibu na korosho (49), visima vifupi vya maji (17), utengenezaji wa matuta nusu duara na uvunaji wa maji ya mvua.

Miradi mingine ni udhibiti wa makongoro, uchimbaji na usafirishaji wa mitaro ya maji, mashamba darasa ya zabibu na korosho pamoja na ujenzi wa barabara.

Alisema wilaya hiyo ina jumla ya vikundi 1,077 vilivyoundwa na walengwa na kila kikundi kina walengwa kati ya 10 hadi 15 kwa ajili ya kuandaa mpango wa biashara ili waendelee kujiinua kiuchumi.