Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541183

Habari Kuu of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: millardayo.com

TBS wametoa vyeti na leseni 246 kwa wazalishaji nchini (+video)

TBS wametoa vyeti na leseni 246  kwa wazalishaji nchini (+video) play videoTBS wametoa vyeti na leseni 246 kwa wazalishaji nchini (+video)

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa jumla ya leseni na vyeti 246 kwa kutumia alama ya ubora wa TBS kwa wazalishaji wa bidhaa nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya amesema kati ya leseni na vyeti 127 sawa na asilimia 51.63 vimetolewa kwa wajasiriamali.

“Vyeti na leseni vilivyotolewa vinahusisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za vyakula,vipodozi,viatu,vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme, magodolo na vifungashio kwa pamoja” Dkt.Ngenya.

Aidha Dkt.Ngenya amesema kuwa leseni na vyeti hivyo vitasaidia bidhaa zilizothibitishwa kukubarika sokoni pamoja na kupata faida kiushindani.

Pamoja na hayo Dkt.Ngenya amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Januari mpaka mwezi Mei mwaka huu, TBS imesajili majengo 3295 ya biashara na kuhifadhi bidhaa za vyakula na vipodozi kwa pamoja pia katika kipindi hicho wamesajili bidhaa 642 za vyakula na vipodozi kwa pamoja.

Kwa upande wake Meneja wa Uthibitishaji ubora TBS, Bw.Gervas Kaisi ametoa wito kwa wazalishaji hao kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa bora wakati wote ili kuendelea kumlinda mlaji na kuunga mkono jitihada za serikali za kuendeleza Viwanda.

Join our Newsletter