Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 08Article 541666

Habari za Afya ya

Chanzo: ippmedia.com

TMDA imeitaka jamii kutambua viashiria vya dawa halisi na bandia

TMDA imeitaka jamii kutambua viashiria vya dawa halisi na bandia TMDA imeitaka jamii kutambua viashiria vya dawa halisi na bandia

Mkurugenzi huyo amezungumza hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa wakaguzi wapya 59 kutoka katika Kanda nane za Mamlaka hiyo yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuzuia mianya ya kuingiza dawa bandia au zisizokuwa na ubora kwa matumizi ya binadamu.

Asemema ili kutambua dawa zote za Antibiotic endapo uzitumia lazima ile harufu ya dawa hiyo baada ya kutumia itatoa harufu katika mkojo wa mtumiaji.

“Kama hutasikia harufu katika dawa hiyo ujue hakuna dawa humo.” amesema Fimbo.

Pia ameongeza kuwa, kwa upande wa dawa za wajawazito za kuongeza damu za Iron (foric acid) , lazima baada ya kutumia dawa hizo kinyesi chake kiwe cheusi kuashiria ni dawa sahihi.

“Kinyesi kisipokuwa cheusi ujue hamna dawa humo ndani ya hiyo dawa. Kila dawa inamatokeo yake baada ya kutumia lakini isipotoa matokeo husika ujue dawa hiyo ni bandia hivyo inatakiwa hatua kuchukuliwa haraka” amesema Fimbo.

Aidha ameongeza kuwa, dawa zote zilizosajiliwa ama zilizokaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za TMDA za usajiri ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi hata hivyo mtumiaji lazima achukue taadhari ya dawa anayotumia kama ni sahihi au ni bandia.

Join our Newsletter