Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 21Article 552832

Habari za Mikoani of Saturday, 21 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

TRA Kagera kukusanya Bilioni 83

TRA Kagera kukusanya bil 83 TRA Kagera kukusanya bil 83

Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera inategemea kukusanya shilingi bilioni 83 kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Afisa msaidizi wa kodi ambaye anasimamia utoaji elimu na huduma kwa mlipa kodi mkoanihumo, Alex Mwambenja ametoa kauli hiyo wakati wa semina kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Bukoba Juu ya mabadiliko ya sheria na kanuni za kodi ili waweze kuyafanyika kazi.

Mwampenja amesema kuwa kiwango hicho wanategemea kukipata kutoka kwa wafanyabiashara na walipa kodi wengine hivyo wanapaswa kuwa tayari kulipa kodi kwa hiari ili kujenga uchumi wa nchi.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha TRA inapanua wigo wa kukusanya kodi, katika mwaka wa fedha 2020/21 wamesajiliwa walipa kodi wapya elfu 3,000 na mpaka sasa zoezi hilo linaendelea .