Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540397

xxxxxxxxxxx of Friday, 28 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

TRA Mwanza yakusanya bilioni 153/- kwa miezi 10

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) kupitia ofisi yake ya mkoa wa Mwanza imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 153 katika kipindi cha Juni, 2020 mpaka Aprili mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Meneja mkuu wa TRA mkoani hapa Joseph Mtandika wakati wa ziara maalumu ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila

Mtandika alisema bado wanaendelea na juhudi za ukusanyaji kodi ambapo kuanzia Mei mosi mpaka Mei 26 wamekusanya Sh bilioni 12.

Alisema katika makusanyo ya Sh bilioni 153, kati yake Sh bilioni 114 ni makusanyo ya kodi za ndani na Sh bilioni 39 ni makusanyo ya forodha.

Alisema lengo lao kutokea mwaka 2015 mpaka 2020 walipanga kuhakikisha wanakusanya Sh trilioni moja lakini walifanikiwa kukusanya Sh bilioni 964.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila amepongeza juhudi za TRA kwa ukusanyaji kodi na kutoa angalizo kwa watumishi wa mamlaka hiyo kutobambikiza kodi zisizo rasmi kwa wafanyabiashara.

Join our Newsletter