Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 21Article 552850

Habari Kuu of Saturday, 21 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Taarifa ya TANESCO kuhusu mafundi wake kufyeka mahindi

Taarifa ya TANESCO kuhusu mafundi wake kufyeka mahindi Taarifa ya TANESCO kuhusu mafundi wake kufyeka mahindi

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema litafanyia uchunguzi suala tukio la Wafanyakazi wa TANESCO kufyeka mazao katika shamba la Mkulima wa Tinde wilaya ya Shinyanga kwa kile kinachodaiwa kuwa amelima katika njia ya umeme ili kubaini iwapo kilimo hicho kimefanyika kwa kuzingatia umbali salama.

Taarifa hiyo ya TANESCO Makao Makuu imesema TANESCO inaendelea kutoa Rai kwa wananchi kutokufanya shughuli za kibinadamu au kiuchumi karibu na miundombinu ya umeme na kwamba wananchi wanatakiwa kuzingatia umbali salama kutoka katika miundombinu ya umeme.SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)UFAFANUZI KUTOKA KATIKA VIDEO IKIONESHA WAFANYAKAZI WA TANESCO WAKIKATA MAZAO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutolea ufafanuzi taarifa kutoka katika video clip ya Agosti 19, 2021 ikionesha Wafanyakazi wa TANESCO wakikata mazao eneo la Tinde mkoani Shinyanga.

Eneo hilo zinapita njia kuu za kusafirisha umeme mkubwa za msongo wa kilovoti 220 kutoka Shinyanga hadi Buzwagi na kilovoti 132 kutoka Shinyanga hadi Tabora.

TANESCO inaendelea kutoa Rai kwa wananchi kutokufanya shughuli za kibinadamu au kiuchumi karibu na miundombinu ya umeme.

Aidha, wananchi wanatakiwa kuzingatia umbali salama kutoka katika miundombinu ya umeme, ambapo umeme wa msongo wa kilovoti 220 umbali unaotakiwa ni mita 60, mita 30 kutoka katikati ya nguzo kuelekea kushoto na mita 30 kuelekea kulia.

Kwa umeme wa msongo wa kilovolti 132 umbali unaotakiwa ni mita 40, mita 20 kutoka katikati ya nguzo kuelekea kushoto na mita 20 kutoka katika ya nguzo kuelekea kulia.

Umbali huu umewekwa kitaalamu kwa ajili ya usalama wa raia pamoja na mali zao, lakini pia usalama wa miundombinu ya umeme ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuwekeza.

TANESCO itafanyia uchunguzi suala hili ili kubaini iwapo kilimo hicho kimefanyika kwa kuzingatia umbali salama kama ulivyoainishwa hapo juu.

Imetolewa na:-

Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makuu