Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 22Article 559108

Habari za Afya of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Taarifa ya WHO kuhusu kupungua wagonjwa na vifo vya COVID-19

Taarifa ya WHO kuhusu kupungua wagonjwa na vifo vya COVID-19 Taarifa ya WHO kuhusu kupungua wagonjwa na vifo vya COVID-19

SHIRIKA  la Afya Duniani, WHO limesema idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na COVID-19 vimeendelea kupungua ulimwenguni katika wiki iliyopita.

WHO imesema leo Septemba 22, kuwa zaidi ya visa milioni 3.6 na vifo chini ya  60,000 vimeripotiwa kati ya Septemba 13 na 19, Kupungua kwa kiasi kikubwa cha visa hivyo kumeripotiwa kwenye nchi za Mashariki mwa Mediterania na Kusini Mashariki mwa Asia.

Aidha India imetangaza kuwa itaanza kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa watoto wenye umri wa miaka 12 au zaidi kuanzia mwezi ujao.

Urusi kwa upande wake imetangaza kuwa takriban watu milioni 40 nchini humo wamepata chanjo kamili ya COVID-19.