Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558832

Habari Kuu of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Taarifa ya Waziri Mkuu kuhusu usambazaji wa maji vijiji vyote Tanzania

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa maji wa Kemondo-Maruku Kagera Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa maji wa Kemondo-Maruku Kagera

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika vijiji vyote nchini kote.

Ametoa kauli hiyo mkoani Kagera mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji wa Kemondo - Maruku ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema kwa sasa Serikali inaendelea kutekeleza kampeni ya Rais Samia Suluhu ya kumtua mama ndoo kichwani, yenye lengo la kuhakikisha huduma ya maji inapatikana katika maeneo ya karibu na kuwawezesha Wanawake hasa wa maeneo ya vijijini wanapata muda wa kushiriki katika shughuli za kijamii.

Akirejerea mradi huo, ameongeza kusema kuwa vijiji vinakavyonufaika na mradi huo ni vya kata za Kemondo, Maruku, Nyangereko, Bujugo na Katerero wilayani Bukoba na kata ya Muhutwe wilayani Muleba.

Aidha Mradi huo unatekelezwa kwa awamu na unakadiriwa kunufaisha Wananchi 117,461 kwa gharama ya shilingi bilioni 15.9.