Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584725

Habari Kuu of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Taasisi ya WYV-Foundation kuvifikia vituo 200 vya watoto yatima

Taasisi ya WYV-Foundation kuvifikia vituo 200 vya watoto yatima Taasisi ya WYV-Foundation kuvifikia vituo 200 vya watoto yatima

Taasisi ya Woman and Youth Voice-Foundation imepanga kuvifikia vituo 200 vya watoto yatima kwa Tanzania Bara na Visiwani huku ikipanga kuanza na vituo 10 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza jana Januari 9, 2022 katika kikao cha kwanza cha mwaka 2022, Mkurugenzi Mkuu wa WYV, Mwanaisha Mndeme alisema hatua hiyo ni miongoni mwa malengo ya taasisi kwa mwaka huu.

Alisema baada ya kuvifikia na kutoa msaada katika vituo hivyo, wataendelea na zoezi hilo kwa mikoa mingine ya jirani.

“Lakini pia tutaangalia na uhitaji wa mkoa husika, kwa mikoa ambayo iko karibu tunaweza kuanza na Tanga au Morogoro, lakini kwa kushirikiana na maafisa maendeleo wanaweza kutusaidia kujua kuna uhitaji kiasi gani kwenye eneo hilo,”ameongeza Mwanaisha.

Amesema lengo lingine ni kuhakikisha wanatoa elimu ya kisheria bure kwa wenye uhitaji na katika kufanikisha hilo wamepanga kufanya makongamano na warsha ili kutimiza lengo hilo.

“Lengo ni kuwafikia watoto wa kike kuwapa ushauri na elimu kuhusu unyanyasji wa kijinsia, kujiamini na kujitambua, pia elimu ya kisheria bure na tutaangalia makundi yote yenye uhitaji maalumu,” alisema Mwanaisha.

Taasisi ya WYV imeanzishwa hivi karibuni ambapo Desemba 16 2021, taasisi hiyo ilitoa misaada mbalimbali kwa kituo cha kulea watoto yatima Hisani Orphanage Center kilichopo Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam