Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540400

Habari Kuu of Friday, 28 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Taasisi za umma zinachangia 39% migogoro ya ardhi nchini- Naibu Waziri Ardhi  

Taasisi za umma zinachangia 39% migogoro ya ardhi nchini- Naibu Waziri Ardhi    Taasisi za umma zinachangia 39% migogoro ya ardhi nchini- Naibu Waziri Ardhi  

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Angelina Mabula amesema taasisi za umma ambazo zinadaiwa fidia ya utwaaji ardhi na wananchi zinachangia asilimia 39 migogoro yote nchini.

Kufuatia hali hiyo, Serikali imezitaka kuacha kuchukua ardhi za wananchi bila kulipa fidia na taasisi zinazodaiwa fidia kulipa mara moja vinginevyo maeneo hayo yatarejeshwa kwa wananchi.

MabulaMabula aliyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Kainja(CCM).

Katika swali lake, Kainja alitaka kujua ni lini serikali itamaliza migogoro ya ardhi katika mikoa ya Tabora na Singida ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa utulivu na amani.

Akijibu swali hilo, Mabula alikiri serikali kutambua uwepo wa migogoro ambayo kwa muda mrefu haikuwa imepatiwa ufumbuzi.

Alisema katika mwaka wa fedha 2020/21, Wizara iliagiza Ofisi zote za Ardhi za Mikoa nchini ikiwemo Singida na Tabora kuanzisha jedwali la migogoro ya ardhi ili kuibainisha na kuitatua.

Alisema kwa Mkoa wa Tabora, jumla ya Migogoro 211 iliorodheshwa na kati ya hiyo migogoro 102 ilipatiwa ufumbuzi.

Aidha, Mabula alisema kwa Mkoa wa Singida jumla ya migogoro 226 imetambuliwa na kati ya hiyo migogoro 34 imetatuliwa na iliyobaki asilimia 85 inatokana na madai ya fidia ambayo wananchi wanadai halmashauri na taasisi mbalimbali za serikali.

Join our Newsletter