Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540118

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Taasisi zadaiwa bilioni 82/- kodi ya ardhi

Taasisi zadaiwa bilioni 82/- kodi ya ardhi Taasisi zadaiwa bilioni 82/- kodi ya ardhi

WIZARA wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema hadi sasa taasisi za umma zinadaiwa Sh bilioni 82 za malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, aliyasema hayo bungeni jana wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Alisema pamoja na juhudi zilizofanyiwa na wizara za ukusanyaji wa maduhuli, Wizara bado inazidai taasisi za umma na jitihada zinaendelea kuhakikisha madeni hayo yanalipwa.

Lukuvi alisema katika

mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara ilipanga kukusanya Sh bilioni 200 kutokana na vyanzo vya mapato ya kodi, ada na tozo za ardhi.

“Hadi kufikia Mei 15, 2021, Wizara imekusanya Sh bilioni 110 sawa na asilimia 55 ya lengo chini ya uratibu wa ofisi za ardhi za mikoa,” alisema.

Aidha, Lukuvi alisema katika mwaka wa fedha 2021/22, Wizara imepanga kukusanya Sh bilioni 260 kutokana na kodi ya pango la ardhi, ada na tozo zinazohusiana na sekta ya ardhi.

Alisema ili kufikia malengo ya kukusanya mapato, Wizara imejipanga kuimarisha miundombinu ya Tehama (teknolojia ya Habari na Mawasiliano) katika ofisi za ardhi za mikoa, kuboresha kanzidata ya wamiliki wa ardhi kwa kutumia mfumo

unganishi wa kielektroniki utakaosaidia kuhifadhi kumbukumbu za ardhi na kuwasiliana na wamiliki kwa kutuma ujumbe mfupi na barua pepe.

Aidha, kuhakiki majina ya wamiliki wa ardhi katika hati zilizosajiliwa ili kuoanisha na taarifa zilizoko katika mifumo mingine ya Serikali ili kuwabaini wamiliki hewa na wasiolipa kodi, pamoja na kufanya uhakiki wa viwanja na mashamba ili kubaini wamiliki waliobadili matumizi na kuwalipisha kodi stahiki.

Lukuvi alisema pia Wizara itashirikiana na serikali za mitaa kusambaza hati za madai, kufuatilia malipo ya madeni na kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi.

“Wizara itaongeza wigo wa makusanyo kwa kuwaha-

masisha wananchi kumilikishwa viwanja vilivyopimwa pamoja na kutambua na kusajili wamiliki wa kila kipande cha ardhi katika maeneo ambayo hayajapangwa na kupimwa,” alisema.

Kwa mujibu wa WazirLukuvi, wizara pia itapima maeneo ya uchimbaji wa madini na kutoza kodi stahiki, kuhakiki matumizi ya ardhi iliyomilikishwa yakiwemo maeneo ya taasisi za umma na za kidini ili sehemu ya ardhi inayotumiwa kibiashara itozwe kodi stahiki.

“Pia kuongeza kasi ya kutambua, kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa kushirikiana na mamlaka za upangaji na kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa wamiliki wa ardhi kulipa kodi kwa wakati,” alisema Lukuvi.

Join our Newsletter