Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540733

Siasa ya

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tabasamu: Nimetishiwa Kuuawa Walinipigia Simu - Video

Tabasamu: Nimetishiwa Kuuawa Walinipigia Simu - Video play videoTabasamu: Nimetishiwa Kuuawa Walinipigia Simu - Video

MBUNGE wa Sengerema (CCM), Hamis Tabasamu amedai kutishiwa kuuawa na watu wasiowajua baada ya kuchangia bungeni kuwa kazi ya kuweka vinasaba lipewe Shirika la Viwango Nchini (TBS) badala ya kufanywa na GFI (Global Fluids International).

Mbunge huyo amesema mapato yanayotokana na shughuli ya uwekaji wa vinasaba yanaweza kusaidia kugharamia miradi ya ujenzi wa barabara za mijini na vijijini unaofanywa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) kama ukifanywa na TBS badala ya kampuni binafsi.

Tabasamu ameeleza kutishiwa huko jana Jumatano Juni 2, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema tayari taarifa ya kutishiwa kuuawa ipo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma na namba za watu waliomtishia amezikabidhi kwa jeshi hilo lakini hadi sasa hajajua suala hilo limefikia wapi.

“Naomba Spika (Job Ndugai) unilinde kwa uzalendo kwa sababu tunatafuta fedha za barabara za Tarura,”amesema.

Join our Newsletter