Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554656

Habari za Mikoani of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: SwahiliForum

Takukuru kuchunguza ujenzi wa ofisi ya DC Masasi

Ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Masasi Ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Masasi

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza ujenzi wa ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Masasi inayojengwa eneo la Mbuyuni.

Luteni Josephine Mwambashi ametoa maagizo hayo wakati akikagua ujenzi wa ofisi ya jengo la utawala halmashauri ya Wilaya ya Masasi.

Luteni Mwambashi amesema ujenzi huo hadi ulipofikia umetumia shilingi milioni 700 huku nyaraka za matumizi ya fedha hizo zikiwa hazionekani.

Amewataka viongozi wanaopatiwa dhamana na serikali ya kusimamia mirdi ya maendeleo kuwa wazalendo ili ilete tija kwa wananchi.