Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552391

Habari Kuu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Takukuru kuwashitaki waliotajwa na PM Majaliwa

Takukuru kuwashitaki waliotajwa na PM Majaliwa Takukuru kuwashitaki waliotajwa na PM Majaliwa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Temeke Dar es Salaam, imesema mpaka jana ingekuwa imewakamata wote wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha katika miradi ya barabara na waliohusika kukopa Sh billion 19 kwa ajili ya ulipaji fidia ujenzi wa miradi.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Temeke, Donasian Kessy alisema hayo alipozungumza na HabariLEO.

Jumapili Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hakuridhishwa na gharama za ujenzi wa miradi ukiwemo ujenzi wa barabara za Kijichi-Mwanamtoti yenye urefu wa kilometa 1.8 iliyogharimu Sh bilioni 5.4 na barabara ya Kijichi-Toangoma yenye urefu wa kilometa 3.25 iliyogharimu Sh bilioni 13.5.

Majaliwa aliigiza Takukuru kuwafikisha mahakamani waliohusika na ubadhirifu wa fedha hizo na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke waliohusika kukopa Sh bilioni 19 kwa ajili ya ulipaji fidia ujenzi wa miradi.

Kessy alisema uchunguzi wa suala hilo umeanza, utakamilika ndani ya muda alioutoa Majaliwa na watuhumiwa watafikishwa mahakamani. Waziri Mkuu aliagiza watuhumiwa wafikishwe mahakamani kabla ya kesho.

“Uchunguzi umeanza na tunaendelea nao kwa kasi kama Waziri Makuu alivyoagiza. Sasa hivi tunawatafuta wahusika kwa sababu walishaachiswa kazi”alisema.

Kessy alisema wahusika wa sakata hilo ni wote waliotajwa na Waziri Mkuu akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi.

Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni aliyekuwa msimamizi wa miradi hiyo ya DMDP aliyemtaja kwa jina moja tu la Edward, mhandisi wa mradi na waliokuwa wanamshauri mkurugenzi.