Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 04Article 540982

xxxxxxxxxxx of Friday, 4 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Takukuru yafunguka zaidi Tuhuma za Sabaya 

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Salum Hamduni, amesema kila wanapoendelea kumchunguza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya tuhuma zinaongezeka.

Kwa mujibu wa Hamduni, Sabaya alikamatwa kwa tuhuma za makosa kadhaa ya jinai yakiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Alisema watu wengine saba wamekamatwa wakituhumiwa kushirikiana na Sabaya.

Akizungumza na HabariLEO jana, Hamduni alisema uchunguzi dhidi ya Sabaya unaendelea na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kuzingatia ushauri atakaoutoa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Alisema tuhuma nyingi dhidi ya Sabaya ni za jinai na matumizi mabaya ya madaraka, lakini kadri upelelezi unavyoendelea makosa dhidi yake yanaendelea kuongezeka.

“Wakati wowote leo (jana) na kesho atafikishwa mahakamani pending on the opinion of DPP. (Kwa kuzingatia ushauri wa Mkurugenzi wa Mashitaka),” alisema Hamduni.

Mei 13, mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alimsimamisha Ole Sabaya kazi ya ukuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Julai 28 mwaka 2018, Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli alimteua Ole Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na Julai 31 mwaka huo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wakati huo, Anna Mghwira alimwapisha.

Join our Newsletter