Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 04Article 540967

Habari Kuu of Friday, 4 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Takukuru yawaonya wakandarasi wababaishaji

Takukuru yawaonya wakandarasi wababaishaji Takukuru yawaonya wakandarasi wababaishaji

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imewaonya wakandarasi wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali ikisema itawachukulia hatua za kisheria ambao kazi zao hatazikidhi viwango.

Hatua za kisheria zitaenda sambamba na kurudia kazi kwa gharama zao wenyewe.

Adhabu hiyo tayari imemkumba mkandarasi M/S Runazi General Supplies Company Limited aliyekuwa akijenga kipande cha Barabara ya Mkurugusi -Msasa wilayani Chato, chenye urefu wa kilomita 1.5.

Akikagua barabara hiyo wiki hii ambayo mkadandarasi aliamriwa kuirudia tangu Desemba mwaka jana baada ya kuoneka iko chini ya kiwango, Mkuu wa Takukuru Mkoa Leonidas Felix alisema waligundua upungufu huo mwishoni mwa mwaka jana.

“Mkandarasi ameirudia barabara hiyo ambayo iko chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) kwa gharama zake ambazo ni Sh milioni 50.”

“Na ilielekezwa kwamba, hadi 30 Mei mwaka huu, iwe imekamilika, tukalisimamia hilo na sasa iko tayari kwa matumizi,” alisema Felix.

Aidha, aliwataka wahandisi wasimamizi wa miradi kutoka taasisi za serikali, ikiwemo Tarura, kutekeleza wajibu wao kwa weledi ili kuondoa upungufu unaojitokeza katika ujenzi wa miradi ya serikali ili kufanikisha azma ya kuboresha miundombinu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Felix, Mkandarasi aliingia mkataba na serikali wa ujenzi wa barabara hiyo chini ya usimamizi wa Tarura, kwa gharama wa Sh milioni 87.3.

Join our Newsletter