Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 12Article 562906

Habari Kuu of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tamisemi yapewa bilioni 535.6 mkopo wa benki ya dunia

Tamisemi yapewa bilioni 535.6 mkopo wa benki ya dunia Tamisemi yapewa bilioni 535.6 mkopo wa benki ya dunia

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema Wizara hiyo imepewa sh bilioni 535.6 sawa na asilimia 41.1 ya fedha zote zilizotolewa na Benki ya Dunia ikiwa ni mkopo wa wa masharti nafuu wenye thamani ya Sh trilioni 2.7

Ummy alisema fedha hizo wamezielekeza katika kutekeleza vipaumbele mbali mbali, ambapo sh bilioni 304 imepelekwa kwenye elimu msingi ambayo ni elimu ya awali, msingi na sekondari,

Pia kwa upande wa Afya zimepelekwa sh bilioni 226.6 katika kujenga vituo vya Zahanati na vituo vya afya vya Halmashauri, wakati sh bilioni 5 zimeelekezwa kuboresha miundombinu ya wafanyabiashara wadogo.