Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 574042

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tamko la Benki ya Dunia baada ya Tanzania kurejesha waliopata ujauzito mashuleni

Benki ya Dunia imeunga mkono tangazo la Serikali ya Tanzania la kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa e Benki ya Dunia imeunga mkono tangazo la Serikali ya Tanzania la kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa e

Benki ya Dunia imeunga mkono tangazo la Serikali ya Tanzania la kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa elimu, vikiwemo vile ambavyo vimewazuia wasichana wajawazito au kina mama wachanga kuhudhuria shule katika mfumo rasmi.

Uamuzi huu muhimu unasisitiza dhamira ya nchi ya kusaidia wasichana na wanawake vijana na kuboresha nafasi zao za kupata elimu bora, ilisema taarifa ya benki hiyo.

Benki ya dunia imesema zaidi ya wasichana 120,000 huacha shule kila mwaka nchini Tanzania. 6,500 kati yao kwa sababu ni wajawazito au wana watoto.

''Benki ya Dunia inaunga mkono kwa dhati sera zinazohimiza elimu ya wasichana na zinazowezesha wanafunzi wote kusalia shuleni.

''Benki inatarajia kutoa miongozo itakayowawezesha wasichana wajawazito na kina mama vijana kuendelea na masomo na itasaidia utekelezaji wake kupitia ushirikiano wetu na Serikali ya Tanzania katika sekta ya elimu. Kuifanya elimu kuwa bora, salama, na kupatikana zaidi ni muhimu ili kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania.'' ilisema taarifa hiyo.

Hapo jana Tanzania ilitangaza rasmi kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa kwasababu ya kupata ujauzito wakiwa shuleni kurejea masomoni kupitia mfumo rasmi.

Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika miaka 60 ya uhuru wa Taifa hilo.

Mbali na wanafunzi waliopata mimba, wanafunzi wengine waliokatiza masomo ya kwa sababu mbalimbali nao wataruhusiwa kurejea katika mfumo huo rasmi.

'Takwimu za elimu zinaonesha kwamba wanafunzi wanaacha shule kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utoro, ujauzito, vifo pamoja na nidhamu, lakini sababu kubwa katika takwimu za utoro shuleni ambapo kwenye shule za msingi ni 100,008 ambapo wanafunzi watoro ni asilimia 93%, mimba ni asilimia ndogo tu, takribani asilimia 5% ya wanafunzi wanaoacha shule, alisema waziri Ndalichako.

Kwa mujibu wa Waziri Ndalichako wanafunzi watakaotaka kurejea shule wataruhusiwa kufanya hivyo ndani ya miaka miwili baada ya kuwa nje ya mfumo rasmi kwa utoro ama kukatiza masomo.

'Yule ambaye matatizo yaliyomsababisha atoke shuleni yatakuwa yamekwisha na anataka kurudi shuleni serikali itampa nafasi na itakuwa ndani ya miaka miwili tangu alipoacha shule', alisemaKwa mujibu wa Waziri Ndalichako wanafunzi watakaotaka kurejea shule wataruhusiwa kufanya hivyo ndani ya miaka miwili baada ya kuwa nje ya mfumo rasmi kwa utoro ama kukatiza masomo.

Tamko jipya la sasa la Serikali ya Tazanzania kuruhusu wanafunzi waliopata mimba na changamoto zingine kurejea masomoni linahitimisha marufuku iliyodumu kwa zaidi ya miaka minne iliyowekwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, hayati John Pombe Magufuli.

Juni 2017 Hayati Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari akisema ndani ya utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shuleni.

Akazitaka taasisi zinazotetea utaratibu wa wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni, kufungua shule zao za wazazi lakini si kuilazimisha Serikali kufanya hivyo.

Kauli ya Magufuli ikazua mijadala na upinzani kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu nchini na nje ya nchi hiyo, wakiona hatua hiyo ni kumnyika haki ya kupata elimu mtoto wa kike.