Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 17Article 558031

Habari Kuu of Friday, 17 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tanzania Yang'ara Ulimwenguni Uhuru wa Kujieleza

Tanzania Yang'ara Ulimwenguni Uhuru wa Kujieleza Tanzania Yang'ara Ulimwenguni Uhuru wa Kujieleza

Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Utafiti cha Pew Research Centre chenye Makao Makuu yake Washington D.C nchini Marekani kimeiorodhesha Tanzania kama moja ya Mataifa machache ulimwenguni yenye kiwango kikubwa sana cha Uhuru wa watu kujieleza (Freedom of speech) mwaka 2021.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2004 kikiwa na miaka 17 ya kubobea kwenye tasnia ya tafiti mbalimbali kubwa duniani, ilitoa taarifa yake baada ya kuuliza maswali watu mbalimbali wa nchi husika.

Ripoti hiyo imeongozwa na Marekani iliyopata alama 5.73 na kuitaja Marekani kama Taifa linaloongoza duniani kwa kupata kura nyingi za kusifika kwa uhuru mkubwa wa watu kujieleza.

Tanzania imeshika nafasi ya 17 duniani kwa kupata alama 4.38 huku ikishika nafasi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini iliyopata alama 4.8. Tanzania kwenye ripoti hiyo imewaacha mbali majirani zake wa karibu ambao ni Kenya iliyopata alama 4.04, Uganda alama 3.47 n.k.

Ripoti hiyo pia imezitaja nchi za Korea Kaskazini, Burma, Turkmenistan, Equatorial Guinea, Libya, Eritrea, Cuba, Uzbekistan, Syria na Belarus kama nchi zinazoongozwa kwa mkono wa chuma kwa watu wake kuminywa nau uhuru wa habari, vyombo vya habari kuminywa, sheria kandamizi, hofu na vitisho vikitawala.

SOURCE ==> https://worldpopulationreview.com/country-rankings/countries-with-freedom-of-speech