Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 15Article 542710

Habari Kuu of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Tanzania kushiriki mkutano wa kimataifa kizazi chenye usawa

Tanzania kushiriki mkutano wa kimataifa kizazi chenye usawa Tanzania kushiriki mkutano wa kimataifa kizazi chenye usawa

Mkutano huo utafanyika Juni 30 hadi Julai 2,2021 mwaka huu Jijini Mexico.

Kupitia kikao hicho Serikali ya Tanzania inaazimia kutoka na rasimu ya utekelezaji wa namna ya kuwawezesha Wanawake kiuchumi pamoja na kuondoa changamoto zinazowakabili zikiwepo za ukatili wa kijinsia, kuboresha haki za kiuchumi, haki za uzazi, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuendana na teknolojia na ubunifu pamoja na kuwa na usawa katika uongozi na ngazi za maamuzi.

Akizungumza leo mkoani Dodoma, katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu, amesema katika jukwaa hilo, Serikali ya Tanzania ilichagua eneo moja la kumjenga Mwanamke kiuchumi.