Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 20Article 558577

Habari Kuu of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Tanzania yapokea malipo ya mashaka kutoka BAT

Tanzania yapokea malipo ya mashaka  kutoka BAT Tanzania yapokea malipo ya mashaka kutoka BAT

Tanzania ni miongoni mwa mataifa 10 ndani ya bara la Afrika yanayopokea malipo yanayotiliwa shaka kutoka katika mfuko wa tumbaku wa Uingereza na Marekani (BAT) kwa zaidi ya miaka mitano ili kushawishi vituo vya sera ya afya pamoja na washirika wengine.

Shirika la usimamizi wa zao la tumbaku duniani, STOP limethibitisha malipo hayo yaliyofanywa na Mfuko huo wa Marekani kwa nchi za Burundi, Congo, Kenya Malawi, Sudani, Uganda, Zimbabwe, na visiwa na Comoro kati ya mwaka 2008 na 2013.

"Hii kampuni inafanya kazi na nchi zaidi ya 170, na imekuwa ikikataa madai yote inayohusishwa nayo katika ufanyaji wake wa kazi" imesema taarifa hiyo

STOP, imesema kuwa madai haya yamethibitishwa kutoka kwa mashuhuda waliotoa taarifa za wazi kwao, pamoja na nyaraka zilizovunja na rekodi za Mahakamani na kikundi cha utafiti wa kudhibiti tumbaku cha chuo kikuu cha Bath kilichopo Marekani.