Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552619

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tanzia: Mama Mkwe wa Mbowe Afariki Dunia

Tanzia: Mama Mkwe wa Mbowe Afariki Dunia Tanzia: Mama Mkwe wa Mbowe Afariki Dunia

MKE wa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwenyekiti wa zamani na Muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei, Mama Johara Ngawiliawi Mtei amefariki dunia hii leo Ijumaa, Agosti 20, 2021 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Mama Mtei ambaye alizaliwa Mei 9, 1942 ni mama wa Dkt. Lilian Mtei ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe.

Taarifa ya Chadema Jimbo la Hai imethibitisha kutokea kwa msiba huo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Johara Mtei mahali pema peponi. AMEN.