Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551161

Habari za Mikoani of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tanzia: Mama wa Waziri Jafo Afariki Dunia

Tanzia: Mama wa Waziri Jafo Afariki Dunia Tanzia: Mama wa Waziri Jafo Afariki Dunia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Selemani Jafo amepata msiba wa kufiwa na mama yake mzazi, aliyefariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi, majira ya saa saba wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Waziri Jafo amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa mama yake alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali yaliyochangiwa na umri wake mkubwa, na kwamba anatarajiwa kuzikwa leo, Kisarawe mkoani Pwani.

“Mama yangu alikuwa mtu mzima kidogo takribani umri wa miaka 83, alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo uti wa mgongo. Hivi karibuni aliugua nikampeleka Hospitali ya Kisarawe akalazwa akapata matibabu, bahati mbaya changamoto ikawa kubwa tukamhamishia Agha Khan ambako umauti umemkuta. Msiba utakuwa Kisarawe hapa nyumbani kwangu hapa Kisarawe ambapo tutamzika leo,” amesema Jafo.