Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540583

Habari Kuu of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tanzia: Mke wa Clatous Chama Afariki Dunia

Tanzia: Mke wa Clatous Chama Afariki Dunia Tanzia: Mke wa Clatous Chama Afariki Dunia

KIUNGO wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Zambia, Clatous Chama (29) amefiwa na mke wake Bi. Mercy Chama. nchini Zambia.Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Wakala wake imeeleza kuwa; “Ni majonzi makubwa, tunasikitika kutangaza kifo cha mke wa mchezaji Clatous Chama, Mercy Mukuka Chama. Mercy hakuwa tu mke wa mteja wetu lakini alikuwa sehemu ya familia yetu pia. Tunapenda kutoa salam za pole kwa familia ya Chama na Mukuka. Mungu awape nguvu na faraja.” Next-Gen Sports Agency, Wakala wa Chama.