Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541420

xxxxxxxxxxx of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tawa yanasa bunduki 24, watuhumiwa 91

MAMLAKA ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Kanda ya Magharibi imekamata bunduki 24 na meno ya tembo manne yenye uzito kilo 21.2 kati ya Aprili hadi Juni, mwaka huu.

Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi, Bigilamungu Kagoma, alibainiahs ahayo kupitia taarifa jana mjini Tabora katika mkutano na waandishi wa habari.

Alitaja aina za bunduki walizokamata kuwa ni SMG 1, Riffle 3, Shotgun 1 na magobore 19.

Kagoma alisema pia walikamata watuhumiwa 91 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuingia hifadhini bila kibali, uwandaji wa wanyamapori, uvuvi haramu, na uharibifu wa mazingira.

Alisema baadhi ya watuhumiwa walifikishwa mahakamani na wawili walikiri kosa na kulipa faini kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi.

Kagoma alisema katika doria hizo pia walikamata risasi 38 za bunduki za aina mbalimbali na goroli 76 za magobole.

Alisema watumuhimwa wawili kati ya hao walikutwa katika Pori la Akiba la Ugalla wakiwa wametoka kuwinda wakiwa na gobole.

Alitoa mwito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Tawa ili kubaini watu wanaoendesha ujangili huku pia akitoa rai kwa majangili kuacha vitendo haramu vya kuwinda wanyama.

Alisema mwananachi anayependa kushirikiana na Tawa kuwafichua majangili katika Kanda ya Magharibi anaweza kupiga simu namba 0800110048.

Alihimiza wakazi wa Kanda ya Magharibi kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya wanyamapori kwa kuwa gharama kwa Mtanzania ni Sh 4,000/= kwa siku.

Join our Newsletter