Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554635

Habari za Mikoani of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Tetemeko la Ardhi laikumba shinyanga, Geita

Tetemeko la Ardhi laikumba shinyanga, Geita Tetemeko la Ardhi laikumba shinyanga, Geita

Mkoa wa Shinyanga na Geita umekumbwa na tetemeko la ardhi lenye nguvu ya kati ya kipimo cha Rishta 4.8 mapema asubuhi ya leo.

Kwa mujibu wa kituo cha kimataifa cha Jiolojia kinachorekodi taarifa za matetemeko ya ardhi na volcano ,tetemeko hilo limetokea majira ya saa kumi na moja na dakika thelathini na tano Alfajiri.

Haya yamethibitishwa, na Mkuu wa Mkoa huo, Dkt Philemon Sengati aliyebainisha kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokea na kuwa tetemeko hilo lilipiga eneo dogo la Mji wa Kahama.