Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 28Article 560203

Siasa of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: Mwananchi

Tofauti ya posho zadaiwa kuwagawa madiwani

Fedha Fedha

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), Murshid Ngeze amesema utofauti wa kiwango cha posho za madiwani ambazo wanapatiwa wakati wa vikao vya halmashauri zinawagawa.

Ngeze amesema hayo Jumanne Septemba 28,2021 wakati wa ufungaji wa mkutano maalum wa jumuiya hiyo.

Amesema posho za vikao zimekuwa zikiwagawa madiwani ambapo baadhi wamekuwa wakilipwa Sh50, 000 hadi Sh60,000 huku ikijulikana kuwa hulipwa Sh40,000, nauli inategemea na umbali anaotoka diwani.

Ngeze amesema suala hilo hupeleka lawama kwa wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri na wakati mwingine hata kusababisha ugomvi baina yao.

Hata hivyo, amemuomba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu kuliangalia jambo hilo ili kuondoa mgawanyiko huo.