Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559942

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Togolani Mavura ameapishwa kuwa Balozi Korea Kusini

Togolani Mavura apishwa kuwa Balozi Korea Kusini Togolani Mavura apishwa kuwa Balozi Korea Kusini

Rais Samia amemuapisha Balozi Mteule Togolani Idriss Mavura kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini na pia amemuapisha Mathew Kilama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Shughuli za uapisho zimefanyika leo Septemba 27 mwaka 2021 katika Ikulu ya Chamwino Dodoma jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu kitaifa kama Makamu wa Rais, DK. Philips Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Balozi Togolani awali alikuwa ni mshauri binafsi wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete katika kipindi cha miaka moitano ya 2010-2015.

Kabla ya uteuzi huu, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini alikuwa ni Matilda Swilla Masuka aliyemaliza muda wake mwaka 2021.