Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552757

Habari za Afya of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tozo kujenga vituo 207 vya afya

Tozo kujenga vituo 207 vya afya Tozo kujenga vituo 207 vya afya

SERIKALI imesema tozo za miamala ya simu zinaenda kujenga vituo 207 vya afya katika Tarafa ambazo hazijawahi kuwa na vituo.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu, ambapo amesema tayari halmashauri 90 zimeshaingiziwa fedha hizo ambazo ni sh bilioni 22.5 kupitia force akaunti na kuziagiza halmashauri hizo kuzipeleka fedha hizo kwenye Tarafa husika na sio kuzikumbatia kwenye halmashauri zao.

“Tuna tarafa 570 katika hizo Tarafa 207 hazina vituo vya afya, na zilizo na vituo haziwezi kutoa huduma ya upasuaji za mama na mtoto, hivyo naelekeza halmashauri kuhakikisha vituo vinajengwa sio ujanja ujanja wa kukarabati vijengwe katika tarafa za katikati ya halmashauri na kama kuna hospital basi kituo kikajengwe kwenye tarafa za pembezoni za kimkakati.”alisema

Alisema awamu hii ya kwanza fedha hizo zitajengwa maabara, kituo cha kuchomea taka na jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

Ummy amesema awamu ya pilli watajenga wadi za wanawake, wanaume, watoto na chumba cha upasuaji .

“Awamu ya kwaza ya fedha zimeshaingia, halmashauri iziamishe na kupeleka kwa tarafa husika, kuna mtindo halmashuri wanazihodhi fedha hizo na kufanya mambo yote, mwongozo wa serikali fedha hizo zitolewe na tarafa zitaunda kamati zao tatu,”alisisitiza

Aidha alisema utaratibu unaotumika ni wa a force akaunti, hivyo mafundi watakaojenga vituo hivyo vya afya watatoka kwenye tarafa au wilaya husika na si vinginevyo, na halmashauri kazi yake itakuwa ni kusimamia tu.