Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552694

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Tozo za Miamala sio michango ya kirafiki, ni sheria"- Waziri wa Fedha

Miamala ya simu Miamala ya simu

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa tozo za miamala ya simu si michango ya kirafiki ni sheria ya Bunge iliyojadiliwa kwa miezi mitatu, na wabunge wameongelea matatizo ya wananchi.

Kauli hii ya Waziri inakuja ikiwa ni siku moja tangu Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipozungumza na wananchi kuhusu uhalali wa tozo hiyo na kusisitiza kuwa tozo hii ipo kwa mujibu na Sheria za Bunge.

Hata hivyo pia Waziri huyo aliwakata ulimi wale wanaojinadi kwa kusema kuwa watumiaji wa miamala ya simu wamepungua kufuatia wingi wa makato kuwa madai hayo hayana ukweli kwani kiwango cha kutumia miamala kipo pale pale.

“Hapa katikati kumetokea maneno mengi sana ambayo ni lazima tuyaweke sawa, Watu wanasema utumaji wa kimiamala (kutuma na kutoa pesa) umeshuka na kanakwamba Watu wameacha kutumia miamala, sio kweli, niwaambie tu kwamba Watanzania wameendelea kufanya miamala na bado inacheza humohumo kwenye miamala Milioni 9 hadi Milioni 10 kama ilivyokuwa hapo awali.