Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541510

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Trilioni 24.74 zatumika mpango wa Bajeti 2020/21

Trilioni 24.74 zatumika mpango wa Bajeti 2020/21 Trilioni 24.74 zatumika mpango wa Bajeti 2020/21

SERIKALI imetumia Sh trilioni 24.74 zimetumika kugharamia utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati wa kuelezea utekelezaji wa Bajeti wakati wa kuwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2021/22.

Alisema katika kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha za umma, Wizara imeendelea kuzingatia taratibu za kutoa, kukagua, kufuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Serikali.

Nchemba alisema hadi Aprili mwaka huu, jumla ya Sh trilioni 24.74 zimetolewa kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Serikali.

Join our Newsletter