Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 13Article 563056

Habari za Mikoani of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Tsh. Bilioni 28.6 zimepelekwa miradi ya maendeleo Geita

Bilioni 28.6 kuboresha miradi Geita Bilioni 28.6 kuboresha miradi Geita

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa Sh28.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Geita.

Amesema kuwa kwa Wilaya ya Chato pekee tayari imeshapokea bilioni 16 kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii kama elimu, maji, afya, ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma muhimu kwa wakati.

"Mkoa wa Geita tayari umeshapokea bilioni 28.6, tayari zimeshasambaza Wilaya zote kwa ajili ya maji, barabara, elimu, afya, na Wilaya ya Chato zimeshaletwa bilioni 16" Waziri Mkuu

Akizungumzia kuhusu changamoto ya upungufu wa watumishi wa sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali inaendelea kuajiri ili kuhakikisha lengo lake la kufikisha huduma bora za afya kwa wananchi linafikiwa.

Kadhalika,ameuagiza uongozi RUWASA wilaya ya Chato uhakikishe kiasi cha shilingi bilioni 5.2 kilichotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji zinatumika vizuri na wananchi wapate huduma hiyo.

Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa mkoa wa Geita kuhakikisha fedha hizo ambazo zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, elimu, barabara na afya zinatumika kama ilivyokusudiwa.