Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572482

Habari Kuu of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tsh.bilioni 50 kupunguza migogoro ya ardhi nchini

Tsh.bilioni 50 kupunguza migogoro ya ardhi nchini Tsh.bilioni 50 kupunguza migogoro ya ardhi nchini

Serikali imetoa mkopo wa shilingi bilioni 50 za kitanzania bila riba kwa Halmashauri zote nchini kwa ajili ya kupanga, kupima na kurasimisha maeneo yote yaliyokuwa hayajafikiwa na mpango mji kwa malengo ya kupunguza migogoro ya ardhi.

Wizara ya Fedha na Mipango itatoa mikopo hiyo kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo itazipeleka moja kwa moja kwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo.

Mpango huu umepagwa kutekelezwa chini ya Wizara kuu tatu ambazo ni Wizara ya Fedha, Ardhi na TAMISEMI.

Nae Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa mpango huo ni endeevu na kuwa tayari umeashaanza kwa halmashauri 55 na kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa awamu ili kuziwezesha halmashuri zote kunufainika na fursa hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, amesema mradi huo ni muhimu katika kumaliza migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema Wizara hiyo itahakikisha kuwa wakurugenzi wa halmashauri 55 wanatumia fedha hizo kupanga na kugawa viwanja.